KUJENGA MTANDAO WA BIASHARA

Mtandao(network) ni muhimu sana katika kujenga biashara yako na katika kujijenga katika kazi/career yako.Mtandao unakusaidia kupata rasilimali, kupata taarifa za masoko, kupata taarifa mbalimabali na kukamilisha mambo yako ki urahisi. Ili kujenga mtandao tunahitaji kufanya mambo yafuatayo:

1.Jenga mahusiano na watu ambao mnaweza kusaidiana  kibiashara au kikazi. Mahusiano yanajengwa kwa kufahamiana na watu kazini na kuwa na mawasilaiano nao.

2.Shiriki katika matukio yatakayo kusaidia kukutanika na watu mfanoSemina,Mikutano,Michezo, Maonyesho, kusali,sherehe za muhimu na chakula cha jioni na vikundi vya msingi. Usijifungie sana.

3. Tengeneza utambulisho wako(Bussiness card) na wa biashara yako(Vipeperushi) na wapatie watu wanaoweza kuwa rasilimali kwako.

4.Tumia njia za kimitandao kuwasiliana na wateja wako, Marafiki na jamii kwa ujumal(Simu,Email,Facebbook,Snapchart,Twiter,Instagram,Blog nk) uwe unajibu ujumbe na kufuatilia mahusiano yako kwenye mtandao.

5. Tengeneza mtandao wa marefa wako (Referees) amabo watakuwa mabalozi wako, watu hawa wanatengenezwa kwa kujenga mahusiano ya karibu na hata kuwaomba wakutangazie biashara yako.

6. Uwe na takwimu/Database ya wateja wako na watu wa karibu. Kila kukiwa na tukio muhimu kama siku kuu au kumbukumbu mbali mbali wasalimu na kuwatakia kila la kheri.

7.Toa huduma nzuri na jenga tabia ya kufuatilia huduma yako inavyopendwa sokoni . Kukiwa na huduma mpya au bidhaa m,pya wajulishe wateja wako.Usikubali ukakpita muda mrefu bila kuwa na kitu cha kukuweka karibu na wateja wako.

8.Kila unapopata fursa jitambulishe vizuri wewe pamoja na biashara yako,kwa wanaotaka zaidi soma kitu kinaitwa Elevator speech kwenye mtandao (http://www.businessballs.com/business-networking.htm) kwa kifupi kama upo sharp dakika tatu za kukutana na mtu kwenye lift zinatakiwa zitoshe  kukutambulisha wewe na biashara yako na kupata mawasilaiano ya muhusika.

9.Jenga tabia ya kusaidia wengine.Kabla ya kupokea jifunze kutoa. Utapata mtandao mkubwa sana.

10. Timiza ahadi zako na uwe mwaminifu katka mahuiano yenu na kuhusu taarifa za wenzako.

IMEANDIKWA NA DR.GOODLUCK URASSA

MKURUGENZI -EFL