MAMBO MATATU MUHIMU YA KUFANYA ASUBUHI ILI SIKU YAKO IWE YENYE MAFANIKIO.

Asubuhi yako ni muhimu sana kwani  jioni yako ni matokeo ya vile ulivyo ianza siku yako. ” Waswahili husema nyota njema huonekana tokea asubuhi”. Kwa leo nimeona tuangalie mambo muhimu matatu ya kufanya saubuhi na mapema ili siku yako ipate kuwa yenye mafanikio.

TAFAKARI/UWAZO (Meditation).Kumbuka kuwa miili yetu ina nafasi kubwa katika kutafakari. Kabla ya kufanya jambo lolote, ni muhimu kutafakari mambo ya  kufanya kwa siku husika. Tafakari namna utakavyo ipangilia siku yako,namna utakavyo ifanya siku yako kuwa yenye Baraka na yenye furaha. Kwa imani yako mtangulize Mungu katika kila jambo ambalo utalifanya au unalo kusudia kulifanya kwa siku husika.

PENDA KUOGA MAJI YA BARIDI (Cold shower).  Maji ya baridi ni muhimu kwa ajiili ya kuchangamsha mwili.Fanya hivyo angalau kwa muda wa  sekunde thelathini kwenye bomba inayotoa maji ya baridi au kwa kujimwagia mwenyewe, Kwa kufanya hivyo utaufanya mwili wako na akili yako vichangamke.

UWE NA MPANGO KAZI(Making lists). Andaa cha kufanya kwa siku  husika au jioni yako kabla ya kwenda kulala. Watu wengi walio fanikiwa huorodhesha chini vitu vya kufanaya, wengi wao huanza na vile vilivyo vya muhimu na kumalizia na visivyo vya muhimu.Kwa kufanya hivyo siku yako lazima iwe yenye mafaniko mazuri.