USIKATE TAMAA, PAMBANA!

NILIJIFUNZA KITU KWENYE MDAHALO WA PILI WA UGOMBEA URAISI WA MAREKANI.

Donald Trump aliulizwa swali la mwisho kuwa ni kitu gani kizuri alichonacho Hillary Clinton ? akasema ” Huyu mama hakati tamaa (“She doesn’t give up”). Kwa kweli pamoja na changamoto nyingi, mama anazidi kupambana¬† hata kama akishindwa, atajihesabu kashinda kwa ujasiri alio uonyesha.

Ujumbe! Usikate tamaa hata kama hali ni ngumu, uwe na mtazamo chanya iwe kazini au kwenye biashara yako pambana hata kama hali ni ngumu. Ukiamini unaweza, unaweza.

Tafadhali mshirikishe na mwenzako ujumbe huu.

Dr. Goodluck Urassa

Mkurugenzi EFL.