- March 4, 2022
- Posted by: admin
- Category: News
No Comments
Baadhi ya wafanyakazi wakiwa wameambatana na Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi Prof. Goodluck Urassa, wameshiriki na kuiwakilisha vyema kampuni ya Enterprise Finance Limited (EFL) katika mbio za marathoni (KILI MARATHON) zilizofanyika leo 27/02/2022 Mjini Moshi. Ushiriki wa mbio hizo umekuwa ni mwendelezo wa utamaduni wa EFL katika kuandaa na kushiriki michezo mbalimbali ili kuimarisha afya za wafanyakazi na jamii nzima kwa ujumla.