- December 4, 2021
- Posted by: admin
- Categories: CSR, Customer Service
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Profesa Goodluck Urassa ameelezea kuwa tofauti na miaka iliyopita ambapo EFL ilizoea kusheherekea wiki ya Huduma Kwa Wateja, kwa sasa itakuwa inafanya hivyo kwa mwezi mzima.
Akifafanua mkakati huo Profesa Urassa alisema kuwa utaratibu huu utawawezesha menejimenti na wafanyakazi kushirikiana katika kujenga na kuendeleza utamaduni wa kuwahudumia wateja na kuwapa kipaumbele.
Kwa mwezi huu tumeweka utaratibu wa kuwatembelea wateja wetu na kujua mahitaji yao, kusikiliza changamoto zao, kutoa ushauri wa kibiashara , kutoa mafunzo ya Ujasiriamali na usimamizi wa fedha kwa wajasiriamali wanaopenda kushiriki na kujenga uwezo wa wafanyakazi kuwahudumia wateja kwa ufanisi, alieleza. EFL pia itajihusisha katika shughuli za kijamii ikiwa ni pamoja na kuandaa michezo mbalimbali kati yake na taasisi nyingine ili kuchangia katika kuimarisha afya za wafanyakazi, wateja na jamii.