EFL Ilizindua Mwezi Wa Huduma Kwa Wateja

EFL Ilizindua Mwezi Wa Huduma Kwa Wateja

EFL imezindua utaratibu wa kusherehekea Mwezi wa Huduma Kwa Wateja kwa kila mwezi wa Kumi. Wakati wa kuzindua utaratibu huo kwa mwaka huu wa 2021, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Profesa Goodluck Urassa alieleza  kuwa tofauti na miaka iliyopita ambapo EFL ilizoea kusheherekea wiki ya Huduma Kwa Wateja, kwa sasa itakuwa inafanya hivyo kwa mwezi mzima wa Kumi. Utaratibu huu ni tofauti na mazoea ya taasisi nyingi zinazosheherekea huduma kwa wateja kwa wiki moja, alieleza.

Akifafanua mkakati huo Profesa Urassa alisema kuwa sababu kubwa ya kutumia mwezi mzima kusheherekea huduma kwa wateja ni kuiwezesha EFL kukamilisha shughuli mbalimbali ilizokusudia kufanya katika kuboresha huduma zake. Pamoja na kuwa EFL imeweka mikakati mbalimbali kuboresha huduma kwa wateja kila siku, utaratibu huu utawawezesha menejimenti na wafanyakazi kushirikiana katika kujenga utamaduni wa kuwahudumia wateja kwa weledi na ubora wa hali ya juu kwa mwezi mzima, alieleza.

EFL imejipanga kuboresha mahusiano yake na wateja na kutoa huduma za ziada kwa wateja wake na jamii kwa ujumla. Kwa mwezi huu tumeweka utaratibu wa kuwatembelea wateja wetu na kujua mahitaji yao, kusikiliza changamoto za wateja wetu, kutoa ushauri wa kibiashara kwa wateja na jamii, kutoa mafunzo ya Ujasiriamali na usimamizi wa fedha kwa wajasiriamali wanaopenda kushiriki na kujenga uwezo wa wafanyakazi kuwahudumia wateja kwa ufanisi, alieleza. EFL pia itajihusisha katika shughuli za kijamii ikiwa ni pamoja na kuandaa michezo mbalimbali kati yake na taasisi nyingine ili kuchangia katika kuimarisha afya za wafanyakazi, wateja na jamii

SHARE[addtoany]