- September 26, 2023
- Posted by: admin
- Categories: CSR, News, Training
Enterprise Finance Limited (EFL) ina utaratibu wa kuendesha semina mbalimbali kwa wafanyakazi na wafanyabiashara. Semina hizi zinalenga kuwaongezea ujuzi utakaowasaidia kukuza biashara zao na kuzalisha ajira nyingi zaidi kupitia biashara zao.
23/09/2023, EFL imeendesha semina maalum juu ya ujasiriamali na uwekezaji kwa wafanyabiashara na wakazi wa Dodoma. Semina hii ilihudhuriwa na wadau mbalimbali wakiwemo wajasiriamali, wafanyakazi, wadau wa kimaendeleo na wanahabari.
Katika Semina hii, mwezeshaji Prof. Goodluck Urassa alisema “kuna changamoto kuu tatu ambazo inatakiwa tuzifanyie kazi ili kuhakikisha biashara zetu zinakua, la kwanza ni katika usimamizi wa biashara, la pili ni kujenga mifumo ya kuendesha biashara na la tatu ni suala la usimamizi wa fedha yaani kusimamia kidogo ulichonacho na uweze kukikuza kiweze kuzalisha zaidi”
Semina hii ilidhaminiwa na wadau mbalimbali wakiwemo: EFL, ROYAL VILLAGE HOTEL, TCCIA na DODOMA MEDIA GROUP.