SEMINA YA UWEKEZAJI NA USIMAMIZI WA FEDHA JIJINI ARUSHA

 

Walengwa;

Semina hii imelenga wafanyabiashara na wafanyakazi ambao ni wateja wa EFL na wasio wateja katika mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Manyara na Dodoma. Semina imekusudia kuwaleta pamoja washiriki wenye uhitaji wa kujenga miradi ya uwekezaji na biashara zao kwa kuwekeza sehemu sahihi na kulinda fedha zao zisipotee. Imewalenga pia wafanyakazi wanaojiandaa kustaafu kutoka katika ajira zao kwa miaka yakaribuni.

Mada kuu zitakazofundishwa zitakuwa kama ifuatavyo:

  1. Uwekezaji katika Miradi ya kibiashara na kuisimamia
  2. Uwekezaji katika Masoko ya Fedha
  3. Kuwekeza katika vyanzo vya kipato tulivu (passive income)
  4. Kusimamia Mikopo na kuzalisha
  5. Bima kwa manufaa ya wafanyabiashara na wafanyakazi

Wawezeshaji wa Semina;

Mafunzo yatawezeshwa na Professor Goodluck Urassa (UDSM), Mr.Clement Z .Kwayu Mkurugenzi wa Bumaco Insurance Co.ltd na Wafanyabiashara mashuhuri watakaokuja kutoa uzoefu wao.

Utaratibu utakotumika kuendesha semina;

Semina hii itaendeshwa kwa njia shirikishi ambapo washiriki watapata nafasi ya kushirikishana uzoefu, kushiriki katika mijadala mbalimbali na kuuliza maswali. Washiriki wataruhusiwa kuleta bidhaa zao, vipeperushi na taarifa nyingine za biashara zao kuzitangaza. Wataalamu wa UTT na bima watakuwepo kwa ajili ya kutoa uzoefu wa uwekezaji na bima, na kujibu maswali ya washiriki. Kwa watakaopenda kuwekeza watapata ushauri na usaidizi ili waweze kuwekeza. Semina hii Inatarajiwa itawawezesha washiriki kujenga mtandao wa kibiashara pia kwa ajili ya kujifunza zaidi.

Kuhusu Gharama

Semina hii imefadhiliwa na EFL na wabia wake kama sehemu ya huduma za Kijamii. Hivyo, hakuna gharama yeyote ya kushiriki

Semina itafanyika katika Hoteli ya Corridor Springs Arusha tarehe 5/10/2024 kuanzia saa 7 mchana.

JISAJILI SASA PIGA SIMU NAMBA;

+255 758 978 736 | +255 677 226 960

AU FUATA LINK https://efl.co.tz/arusha-training/



Leave a Reply