- March 11, 2024
- Posted by: admin
- Categories: Events, News, Social
Enterprise Finance Limited (EFL) imeungana na Dunia katika kusherehekea siku ya wanawake Duniani 2024. Katika maadhimisho hayo EFL ilifanya mafunzo maalum kwa ajili ya wanawake ili kuwaongezea ujuzi katika masuala ya kiuchumi na kijamii. Muwezeshaji wa mafunzo hayo Prof. Neema Mori kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam aliwahasa wanawake kuanza na uwekezaji binafsi akiakisi kauli mbiu ya mwaka huu isemayo “Wekeza Kwa Wanawake, Kuharakisha Maendeleo ya Taifa na Ustawi wa Jamii”.
Katika hafla hiyo EFL ilimtambulisha Bi. Basileke Hellen Mwansasu ambaye atashiriki Mafunzo ya Ujasiriamali na Usimamizi wa Biashara kwa Wanawake katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Mafunzo haya yatafanyika katika chumba cha mikutano cha CE (UDSM), kuanzia tarehe 14 Machi hadi tarehe 5 Aprili 2024.
Mkurugenzi Mtendaji wa EFL Bi. Jacqueline Lujuo alimshukuru Prof. Mori kwa kujitoa kwake kufika katika mafunzo hayo maalum lakini pia alimpongeza Bi. Basileke ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Alpha Quality Service kwa kupata nafasi ya kujifunza na kusisitiza kuwa mafunzo ni endelevu.