Wafanyakazi wa EFL tawi la Arusha wakishiriki mafunzo kwa vitendo.

Ikiwa ni mwendelezo wa kuboresha huduma bora kwa wateja, wafanyanakazi  wa kampuni ya Enterprise Finance Limited ( EFL) tawi la Arusha wameshiriki  mafunzo kwa vitendo yaliyolenga kuboresha na kudumisha ushirikiano katika utendaji kazi ili kuendeleza utamaduni wa kampuni wakutoa huduma bora kwa kuzingatia mahitaji ya mteja.