- October 15, 2024
- Posted by: admin
- Categories: Events, News
Enterprise Finance Limited (EFL) imetoa msaada wa mahitaji mbalimbali katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road iliyopo Dar es Salaam. EFL imekuwa na utaratibu wa kugusa jamii kwa namna mbalimbali katika kipindi cha wiki ya huduma kwa wateja, ikiwemo mafunzo ya bure kwa wajasiliamali, zoezi la upandaji miti, mbio za hisani, kufanya usafi katika fukwe n.k.
Akizungumza na waandishi wa Habari Meneja wa Sheria na Afisa Uhusiano Bw. Denis Lyimo amesema utaratibu huo wa kampuni umekuwa desturi na endelevu ikiwa ni sehemu ya kuwajibika kwa jamii yaani Corporate social responsibility.
Nae Afisa Muuguzi Mkuu katika Taasisi hiyo Brigita Mapunda ameishukuru EFL kwa kuchagua Ocean Road kuwa sehemu ya kufikisha msaada huo aidha ametoa rai kwa makampuni mengine kuiga utaratibu huo kwani uhutaji ni mkubwa sana.