- October 14, 2020
- Posted by: admin
- Categories: Community Involvement, CSR, Customer Service, Training
Kampuni ya Enterprise Finance limited imeungana na ulimwengu mzima kwa kutoa heshima kwa wateja na wafanyakazi wa kampuni yake ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya kimataifa ya huduma kwa wateja inayofanyika kila mwezi oktoba, wiki imehusisha shughuli mbalimbali kama vile mafunzo,michezo, kutembelea wateja katika biashara na ofisini pamoja na kupata mrejesho kuhusu huduma zinazotolewa.
Wateja wametoa pongezi kwa wafanyakazi na EFL kwa ujumla kwa kutambua namna wanavyojituma kutoa huduma kwa haraka, weledi na uaminifu mkubwa. EFL imeahidi kuendeleza kuboresha zaidi huduma zake kuwa za haraka zaidi na kuhudumia wateja kulingana na mahitaji yao.
Baada ya mafunzo ya vitendo yaliyolenga kuboresha na kudumisha ushirikiano wakati wa kuhudumia wateja yaliyofanyika Ndoto polepole farm Bagamoyo (kama inavyonekana kwenye picha hapo juu), Mkurugenzi Mtendaji Ndugu. Jacqueline Lujuo alitumia fursa hiyo na kufafanua kuwa huduma bora inayotolewa na EFL inatokana na juhudi za kila wakati za kutafuta njia mpya za kuwahudumia wateja wake kwa haraka, weledi ili kukidhi mahitaji na matarijio yao wakati wote, hivyo amewasihi wafanyakazi kuendeleza utamaduni huo ili kujenga taasisi ya kifedha yenye nguvu zaidi nchini.