WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA

Enterprise Finance Limited imeandaa wiki ya huduma kwa wateja ambayo itafanyika kuanzia tarehe 10-15 October 2016. Msimu huu tumepanga kuwafikia wateja wengi zaidi ikiwa ni pamoja na kutoa huduma bora zaidi. Masharti yameboreshwa zaidi ili kuwafikia wote wenye uwezo wa kupata mkopo.

Vile vile tunahitaji maoni yako ili kuboresha zaidi.Unaweza kututumia kwa email ambayo ni info@efl.co.tz. Pia katika kusherehekea wiki hii kutakuwa na burudani mbalimbali ikiwa ni pamoja na michezo ya aina mbalimbali. Tutakuwepo katika viwanja vya Mapambano Siku ya A lhamisi ya Tarehe 13/10/2016. Tunawakaribisheni nyote wapenzi wa michezo, ili tuweze kufurahi kwa pamoja.