EFL ILIANDAA BONANZA YA MICHEZO KAMA NJIA YA KIPEKEE KUADHIMISHA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA

Katika juhudi ya kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja, EFL iliandaa kitu cha kipekee na tofauti kabisa kama ilivyozoeleka huku ikelenga kuleta jamii pamoja,kujenga mahusiano mema, kuboresha afya, kuhamasisha umuhimu wa michezo n.k.
Hivyo basi katika kutekeleza hayo, EFL iliandaa BONANZA ya michezo mbalimbali ikiwemo kukimbia mbio fupi fupi (km 5 na km 10) zijulikanazo kama EFL Fun Run 2022, mbio hizi zitajumuisha familia pia, Mashindano ya mpira wa miguu (soka), na michezo mingine kadha wa kadha.
Michezo hii ilifanyika tarehe 15/10/2022 katika viwanja vya Chuo Kikuu Dar es Salaam, kuanzia saa 12:00 Asubuhi mpaka 6:30 Mchana.
Bila kiingilio, wote walikaribishwa kujumuika pamoja.