EFL ILISHIRIKI MAONYESHO YA BIASHARA (SABASABA) 2022

Katika kuelekea ufunguzi wa maonyesho ya biashara ya kimataifa  yaani sabasaba, yanayoandaliwa na TANTRADE kila mwaka, ENTERPRISE FINANCE LIMITED (EFL), imejipanga vizuri kushiriki maonyesho hayo ambayo yanatarajia kuanza rasmi tarehe 28 June Mpaka 13 July 2022. Lengo la kushiriki maonyesho hayo ni pamoja na kukuza na kuboresha upatikanaji wa huduma ya kifedha kwa kuwafikia wadau wengi ambao bado wanauhitaji wa kupata mitaji ya kukuza/kuboresha biashara zao . Juhudi hizi zinakwenda sambamba na sera ya serikali inayolenga kukuza na kulinda wafanyabiashara Tanzania.

Hivyo idara ya masoko itakuwepo muda wote ili kutoa elimu zaidi juu ya mikopo mbalimbali inayotelewa na EFL.