EFL ILITOA SEMINA YA BURE KWA WAKANDARASI

Enterprise Finance Limited (EFL), ni kampuni inayojishughulisha na utoaji wa mikopo ya haraka kwa masharti nafuu ndani ya muda wa saa 48 ikilenga kutatua dharura mbalimbali za kifedha , pia EFL imejikita katika utoaji wa mafunzo ya ujasiriamali ili kukuza biashara ya wateja na wadau wake wote.

Katika kutambua mchango mkubwa unaotolewa na wakandarasi katika jamii yetu, EFL iliandaa semina ya bure kwa Wakandarasi wote,  iliyolenga kukuza kampuni, usimamizi wa miradi na  fedha pamoja na kutoa fursa za mikopo ya kuendeleza/kufanya miradi. Semina ilifanyaka tarehe 03/09/2022 katika jengo la EFL House, Sinza, Africa sana  kuanzia Saa 4:00 Asubuhi –  Saa 10: Jioni.

Washiriki walitakiwa kujaza taarifa zako kwa kutembelea link hii https://efl.co.tz/usajili-wa-semina/ au kwa maelezo zaidi kupiga simu 0758 112 332/0677 111 333